Rayvanny

Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania kutoka WCB Wasafi Record label


Raymond Shaban Mwakyusa (anafahamika zaidi kwa jina lake kama Rayvanny; amezaliwa 22 Agosti 1993) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania (kwa asili ni mtu wa mkoani Mbeya).

Rayvanny
Jina la kuzaliwaRaymond Shaban Mwakyusa
Pia anajulikana kamaRayvanny
Amezaliwa22 Agosti 1993 (1993-08-22) (umri 30)
Asili yakeMbeya,Tanzania
Aina ya muzikiBongo Flava,Afro Pop
Kazi yakeMwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
AlaPiano, sauti
Miaka ya kazi2011–mpaka sasa
StudioWasafi Records,Next Level Music
Ame/Wameshirikiana naHarmonize, Diamond Platnumz
TovutiRayvanny

Wasifu

"Rayvanny" alianza kujulikana kupitia wimbo wake "Kwetu"[1] si siku nyingi sana tangu Harmonize atoe wimbo wake wa Bado.

Baadaye Natafuta Kiki, Sugu ambayo imetolewa kama wimbo wa ziada tu hasa ukizingatia umechukua biti ya Bow Wow (What's My Name). Halafu Mbeleko, Shikwambi, Zezeta na Kijuso aliyoimba na Queen Darleen, Pochi Nene aliyoimba na s2kizzy na baadaye Mwanza wimbo ambao aliimba na msanii mwenzie Diamond Platnumz. Wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa nchini Tanzania BASATA kutokana na kutokuwa na maadili mema hivyo kufanya wimbo huo kufungiwa kupigwa kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.

Baada ya wimbo huo kufungiwa yeye na Diamond walitoa wimbo uitwao Tetema, wimbo ambao ulipendwa na watu wengi kuufanya kuwa na watazamaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mfupi sana.

Albamu

NYIMBO
NambariMada ya wimboMwakaTan[2]
1."Kwetu"2016
2."Natafuta Kiki"2016
3."Sugu"2017
4."Mbeleko"2017
5."Shikwambi"2017
5."Zezeta"2017
6."Chuma Ulete"2017
7."Unaibiwa"2017
Nyimbo za kolabo
NambariMada ya WimboMwakaMwanamuziki mkuuTan
1."Salome"2016Diamond Platnumz
2." Kijuso"2017Queen Darleen[3]
3."Zilipendwa"2017Rich Mavoko, Diamond Platnumz, Mbosso, Harmonize, Lavalava, Queen Darleen[4][5][6]
1."Cuppy jollof on the jet"2020Rema

Tanbihi

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rayvanny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.