Viktoriano Pio

Viktoriano Pio (San Milian de Lara, Burgos, 7 Julai 1905 - Turon, 9 Oktoba 1934) alikuwa bradha wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana katika shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo.

Aliuawa kwa imani yake pamoja na wenzake 7 (Sirili Bertran, Marchano Yosefu, Benjamini Juliani, Juliani Alfredo, Augusto Andrea, Benito wa Yesu na Aniseto Adolfo[1][2]) na padri Mpasionisti Inosenti wa Imakulata wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Aprili 1990, halafu mtakatifu tarehe 21 Novemba 1999.

Sikukuu inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.