Waashuru

Waashuru (kwa Kiaramu ܣܘܪܝܝܐ) ni kabila la Kisemiti la watu wa Mesopotamia kaskazini, ambao leo kwa kiasi kikubwa wanaishi nje ya nchi yao asili (hasa katika Iraq na Syria za leo, pamoja na maeneo madogo ya Uturuki na Iran), hasa Marekani, Ulaya Magharibi na Australia.[1][2][3][4][5][6]

Ukumbusho wa maangamizi ya Waashuru yaliyofanywa na Waturuki mwanzoni mwa karne ya 20; uko Yerevan, Armenia.

Kwa jumla duniani kote wanakadiriwa kuwa kati ya milioni 2 na 4.25. Wengi wao ni Wakristo (hasa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Kanisa la Waashuru la Mashariki), na kwa sababu hiyo wamedhulumiwa na watawala mbalimbali kwa karibu miaka 2000 mfululizo.[7]

Waashuru wana historia tukufu upande wa ustaarabu na siasa kwa kuwa walirithi na kueneza utamaduni wa Wasumeri na Waakadi ambao ndio wa kwanza duniani katika mambo mengi.

Hasa dola la Ashuru lilistawi kati ya karne ya 24 KK na karne ya 7 KK liliposhindwa na Wakaldayo wa Babuloni (605 KK).

Biblia inazungumzia mara nyingi habari za dola hilo lililokuwa tishio kwa Waisraeli na mataifa mengi ya Mashariki ya Kati kwa muda mrefu.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waashuru kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.