Wahan

Wahan (kwa Kiing. Han Chinese) ni kundi la kimbari lenye asili katika Asia ya Mashariki. 92% za watu wa China ni Wahan, kwa jumla ni bilioni 1.4[1]. Kati ya watu wote duniani, 19% ni Wachina wa Han. Wachina wa Han wana viwango vya juu zaidi katika Mikoa ya Mashariki ya China, haswa katika mikoa ya Hebei, Jiangsu na Guangdong. Kuna milioni kumi kadhaa za Wahan nje ya China yenyewe, wengi wao wanaishi Asia ya Kusini-Mashariki.

Mume na mke wa Kihan wakiwa wamevaa nguo za kiutamaduni.

Asili ya Wahan walikuwa makabila katika kaskazini ya nchi yaliyolima kwenye maeneo ya Mto Njano[2]. Makabila hayo yalikuwa pia msingi wa milki za nasaba za kwanza.

Makabila ya Wahan yaliendelea kuenea katika China ya Kusini kwa njia ya walowezi waliotafuta mashamba mapya na uvamizi wa kijeshi. Makabila mengi ambayo hayakuwa Wahan kiasili yalipokea utamaduni na lugha ya Wahan.

Jina la "Wahan" lilianza kutumiwa wakati wa nasaba ya Han.[3]

Marejeo

Viungo vya Nje