Zirikoni


Zirikoni ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 40 katika mfumo radidia. Hutokea ndani ya mitapo na rangi yake ni nyeupe-kijivu ikisafishwa.

Zirikoni (Zirconium)
Fuwele za Zirikoni tupu
Fuwele za Zirikoni tupu
Jina la ElementiZirikoni (Zirconium)
AlamaZr
Namba atomia40
Mfululizo safuMetali ya mpito
Uzani atomia 91.224
Valensi2, 8, 18, 10, 2
Densiti6.52
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka2128 K (1855 °C)
Kiwango cha kuchemka4682 K (4409 °C)
Asilimia za ganda la dunia0.016 %
Hali maada mango


Tabia

Hutokea katika mitapo ya miamba kama graniti na zaidi kama mashapo. Kwa kawaida hutokea pamoja na elementi ya Hafni. Ni metali ngumu inayofanana na Titani haibabuiki kirahjisi.

Huchimbwa hasa Australia na Afrika Kusini.

Matumizi

Matumizi yake ni hasa katika teknolojia ya tanuri nyuklia hasa kama koti za nondo za urani ndani ya tanuri nyuklia. Tabia ya kutobabua kirahisi imesababisha pia matumizi yake katika aloi za feleji za pekee kwa mfano kwa ajili ya vifaa vya upasuaji.


Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zirikoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.