Rafaela Maria wa Moyo Mtakatifu

Rafaela Maria wa Moyo Mtakatifu (jina la kuzaliwa: Rafaela Porras Ayllón; Pedro Abad, Córdoba, 1 Machi 1850 - Roma, Italia, 6 Januari 1925) alikuwa bikira wa Hispania aliyeanzisha pamoja na dada yake shirika la Wajakazi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Mt. Rafaela Maria

Aliliongoza kama mkuu wa kwanza hadi alipong'atuka mwaka 1893. Akidhaniwa amerukwa na akili, alivumilia hadi mwisho mateso na dharau kama toba yake[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1952 halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 23 Januari 1977.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[3].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.