Rhine

Rhine (tamka: rain) (kwa Kijerumani Rhein, Kifaransa Rhin na Kiholanzi Rijn) ni kati ya mito mirefu ya Ulaya.

Rhine (Rhein)
Rhine katika Ujerumani kwenye mwamba wa Loreley
ChanzoGrisons (Uswisi)
MdomoBahari ya Kaskazini katika Uholanzi
NchiUswisi, Liechtenstein, Austria, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi
Urefu1,230 km
Kimo cha chanzo2,344 m
Tawimito upande wa kuliaNeckar, Main, Lahn, Ruhr, Lippe
Tawimito upande wa kushotoAare, Ill, Mosel
Mkondo2230 m³/s
Eneo la beseni185,000 km²
Miji mikubwa kando lakeBasel, Strassburg, Karlsruhe, Mannheim, Ludwigshafen, Wiesbaden, Mainz, Koblenz, Bonn, Köln, Leverkusen, Düsseldorf, Neuss, Krefeld, Duisburg, Nimwegen, Rotterdam, Arnheim, Utrecht, Leiden

Chanzo na nchi inapopita

Ramani ya Rhine

Ina chanzo chake katika milima ya Uswisi. Inapita katika Uswisi, Ujerumani na Uholanzi; mwendo wake ni pia mpaka kati ya Uswisi na Liechtenstein, Uswisi na Austria halafu Ujerumani na Ufaransa.

Mpakani kati ya Uswisi na Ujerumani mto inapita katika ziwa la Konstanz (au: Bodensee).

Njia ya maji

Kuanzia mji wa Rheinfelden hadi Rotterdam kwa urefu wa zaidi ya 800 km mto unapitika kwa meli za mtoni.

Usafiri mtoni ni muhimu kwa ajili ya viwanda vingi vilivyopo kando la mto.

Kihistoria Rhine pamoja na mto Danubi ilikuwa mpaka wa kakazini ya Dola la Roma.

Delta ya Rhine

Ndani ya Uholanzi mto hujigawa kuwa na mikono mikubwa miwili inayoitwa Waal na Lek. Mbele ya mji wa Rotterdam inaungana tena kuwa mto mmoja.

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rhine kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.