Chanjo ya kipindupindu

Chanjo ya kipindupindu ni chanjo madhubuti katika kuzuia kipindupindu.[1] Zinatenda vizuri 85% muda wa miezi sita wa kwanza na 50-60% muda wa mwaka wa kwanza. [1][2][3]

Uponaji wake unapungua hadi kasoro 50% baada ya muda wa miaka miwili. Endapo asilimia kubwa ya idadi ya watu wa nchi moja imepata kinga madhubuti maslahi kutoka kwa kinga kuwepo kwa walio wengi, pengine yanatokea miongoni mwa wale wasio na kinga madhubuti. Shirika la Afya Duniani linapendekeza matumizi yao pamoja na mkusanyo wa namna za tiba nyingine kwa wale wenye hatari kubwa ya kuambukizwa. Dozi mbili au tatu ya aina ya kumezwa kwa kawaida zinapendekezwa. [1] Aina ya kudungwa sindano inapatikana maeneo mengine ya dunia bali upatikanaji wake si sawa na ile ya kumezwa. [2][1]

Usalama

Aina zote mbili za chanjo za kumezwa hazina hatari, ni salama.[1] Maumivu yasiyo makali ya fumbatio au kuharisha huenda yatatokea. Ni salama kwa akina mama waja wazito pamoa na wenye upungufu wa kingamwili.

Zimesajiliwa kutumika katika nchi zaidi ya 60. Zinatumika katika nchi ambako maradhi hutokea kwa wingi na bei ni nafuu. [1]

Jamii na utamaduni

Chanjo za kwanza zilizotumiwa dhidi ya kipindupindu ziliundwa katika enzi za mwisho za 1880. Zilikuwa za kwanza kutumiwa katika maeneo mengi ya dunia ambazo zilitengenezwa katika maabara. [4]

Chanjo za kumezwa zilitumiwa kwa mara ya kwanza katika enzi za 1990.[1] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Duniani, dawa muhimu sana katika mfumo wa afya.[5]

Bei ya kinga dhidi ya kipindupindu iko kati ya dola za Marekani 0.1 na 4.0[6]

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya kipindupindu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.