Siku ya Mama

sherehe ya kuwaenzi akina mama

Siku ya Mama ni sikukuu ya maadhimisho ya kuonyesha heshima na thamani ya akina mama katika familia kutokana na mchango na ushawishi wao mkubwa katika jamii. Siku hii husherehekewa katika tarehe tofauti tofauti duniani lakini miezi maarufu zaidi ni ile ya Machi na Mei.

Moja ya picha maarufu za Marekani ikimuonesha Florence Owens Thompson, mama wa watoto saba, akiwa na miaka 32, huko Nipono, California, Machi 1936, akitafuta kazi au msaada wa kijamii ili kuitunza familia yake.

Siku ya Mama ya kisasa ilianza kusherehekewa nchini Marekani mapema kabisa katika karne ya 20.

Siku hiyo haihusiani moja kwa moja na siku ya Mama iliyokuwepo katika jamii nyingine kwa miaka mingi iliyopita hata maelfu ya miaka iliyopita. Kwa mfano katika tamaduni za Wagiriki kulikuwa na siku inayofanana na siku ya mama inayoadhimishwa katika miaka hii ya karibuni, na huko Roma walikuwa na siku yao iliyojulikana kama Hilaria.

Baadaye katika baadhi ya nchi ya Ulaya (hasa Visiwa vya Britania) Wakristo walianzisha Jumapili ya Mama Kanisa iliyokuwa ikiadhimishwa kwa ajili ya kutukuza na kupa heshima Kanisa kama mama wa waumini lakini baadaye ikaelekea kuheshimu akina mama pia[1][2][3][4] Hata hivyo, katika nchi hizo, siku ya mama bado inategemea desturi hizo za kale.[5]

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siku ya Mama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.