Volti

Volti ni kizio cha umeme tuli au kani mwendoumeme ambao ni tofauti ya utuli baina ya mahali pawili kwenye waya kipitishio na huchukua mkondo usiobadilika wa ampea 1 kama nguvu kati ya sehemu pawili ni wati moja.

Mita za aina hii hupima volti kati ya mahali pawili
Beteri za 1.5 V
Nyaya hizi hubeba umeme kwa volti zaidi ya 1000

Kifupi chake ni V.

Fomula yake ni

Maana yake volti moja ni sawa na hisa ya wati 1 gawanya kwa ampea 1.


Volti ni kipimo cha SI. Jina limetolewa kwa heshima ya mwanafizikia Alessandro Volta kutoka Italia.

Ngazi za volti

Viambishi awaliDesimali
µV 1  (mikrovolti)V 0,000 001
mV 1  (milivolti)V 0,001
V1 (volti)V 1
kV 1  (kilovolti)V 1 000
MV 1 (megavolti)V 1 000 000
GV 1 (gigavolti)V 1 000 000 000