Hidrokaboni

Hidrokaboni ni aina mbalimbali za kampaundi ogania za kikemia zinazojengwa kwa atomi za hidrojeni na kaboni pekee.

Molekuli ya methani ambayo ni hidrokaboni aina ya alkani.

Kwa asili zinapatikana hasa katika mafuta ya petroliamu iliyotokana na mchakato wa kuoza kwa mimea na mata ogania yenye kaboni na hidrojeni nyingi. Hidrokaboni haziwezi kuingia katika mmenyuko wa kikemia na maji.

Hidrokaboni ni chanzo muhimu cha nishati kwa binadamu duniani; petroli na diseli ni mchanganyiko wa aina za hidrokaboni.

Vikundi vya hidrokaboni

Hidrokaboni hupangwa katika vikundi 5.

Alkani

Makala kuu: Alkani

Alkani ni hidrokaboni za msingi. Fomula yake ni CnH2n+2.

Jina la alkaniFomula
MethaniCH4
EthaniC2H6
PropaniC3H8
ButaniC4H10
PentaniC5H12
HexaniC6H14
HeptaniC7H16
OktaniC8H18
NonaniC9H20
DekaniC10H22

Alkeni

Alkeni hufanana na alkani lakini zina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni. Fomula yake ni CnH2n.

Jina la alkeniFomula
EtheniC2H4
PropeniC3H6
ButeniC4H8
PenteniC5H10
HexeniC6H12
HepteniC7H14
OkteniC8H16
NoneniC9H18
DeseniC10H20


Alkini

Makala kuu: Alkini

Alkini zina muungo wa mara tatu kati ya kaboni na kaboni. Fomula yake ni CnH2n-2

Jina la alkiniFomula
EthiniC2H2
PropiniC3H4
ButiniC4H6
PentiniC5H8
HexiniC6H10
HeptiniC7H12
OctiniC8H14
NoniniC9H16
DesiniC10H18

Sikloalkani

Makala kuu: Sikloalkani

Sikloalkani ni isomeri za alkeni. Fomula yake ni pia (CnH2n) lakini hazina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni.

Jina la SikloalkaniFomula
SiklopropaniC3H6
SiklobutaniC4H8
SiklopentaniC5H10
SiklohexaniC6H12
SikloheptaniC7H14
SikloctaniC8H16
SiklononaniC9H18
SiklodekaniC10H20


Alkadini

Makala kuu: Alkadini

Alkadini zina muungo jozi mbili kati ya kaboni na kaboni. Fomula ni CnH2n-2. Hizi ni isomeri za Alkini.

Hidrokaboni aromatiki

Hidrokaboni aromatiki ni molekuli ogania yenye umbo la mviringo tambarare. Fomula yake ni CnH2n-6 na "n" ni sawa na kubwa kuliko 6.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hidrokaboni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.