Shira (nyota)
Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Shira
Kundinyota | Mbwa Mkubwa (Canis Major) |
Mwangaza unaonekana | -1.46 |
Kundi la spektra | A0 mA1 |
Paralaksi (mas) | 379.21 ± 1.58[2] mas |
Umbali (miakanuru) | 8.6 |
Mwangaza halisi | 1.43 A – 11.43 B |
Masi M☉ | 2.12 A, 0.97 B |
Nusukipenyo R☉ | 1.7 A – 0.008 B |
Mng’aro L☉ | 25.4 A – 0.027 B |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 9900 A – 25193 B |
Muda wa mzunguko | siku 5.5 |
Majina mbadala | α Canis Majoris (α CMa), 9 Canis Majoris (9 CMa), HD 48915, HR 2491, BD−16°1591, GJ 244, LHS 219, ADS 5423, LTT 2638, HIP 32349 |
Shira (ing. na lat. Sirius si-ri-us, pia α Alpha Canis Majoris, kifupi Alpha CMa, α CMa) ni nyota angavu zadi katika kundinyota ya Mbwa Mkubwa (Canis Major). Ni pia nyota angavu kabisa kwenye anga ya usiku. Mwangaza unaoonekana ni -1.46 mag.
Jina
Shira ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الشعرى اليمانية ash-shi’ra al-yamaniya ambalo linamaanisha “nyota inayoonyesha upande wa Yemen = Kusini”[2]. Hapa Waarabu wanatumia jina la utamaduni wao ingawa walitafsiri pia jina la Kigiriki Κύων Ki-on yaani mbwa waliokuta kwa Ptolemaio katika kitabu chake cha Almagesti. Hivyo kulikuwa zamani pia kwa Kiarabu jina la "nyota ya mbwa" kwa ajili ya Shira. Asili ya jina la Kiarabu الشعرى ash-shi'ra inaweza kutoka kwa Kigiriki Σείριος sei-ri-os inayomaanisha "ya kuchoma, moto sana". Wagiriki walitumia jina hili pamoja na "Nyota ya Mbwa" kwa sababu wakati ule nyota hii ilianza kuonekana vema kwenye anga ya asubuhi katika siku za joto kuu. Hapo kulitokea pia jina la "siku za mbwa" (ing. dog days) kwa ajili ya kipindi cha siku za joto katika lugha mbalimbali.[3]
Katika matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulichagua "Sirius"[4].
Tabia
Shira - Sirius ina mwangaza unaoonekana wa -1.46 mag na mwangaza halisi ni 1.43. [5]. Ni nyota ya karibu na umbali wake na Dunia ni miakanuru 8.60 [6].
Shira si nyota 1 tu bali nyota maradufu. Tangu karne ya 19 inajulikana ya kwamba hapa kuna nyota kubwa inayoitwa sasa Sirius A pamoja na nyota ndogo Sirius B. Zote mbili zinashikamana zikizungukuka kitovu cha graviti cha pamoja (ing. barycenter). Vipimo vya mwendo wa Shira B vinaonyesha uwezekano wa kuwepo kwa nyota ndogo ya tatu lakini Shira C haikuthibitishwa bado.[7] Shira A na B zinazungukana kwa umbali kati ya vizio astronomia 8.2 na 31.5.
Masi ya Shira A ni M☉ 2.02 na nusukipenyo chake R☉ 1.711 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) [8].
Masi ya Shira B ni M☉ 1.02 na nusukipenyo chake R☉ 0.0084.
Tanbihi
Viungo vya Nje
- Constellation Guide: Sirius
- Sirius (Alpha Canis Majoris), "Stars", kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
- Star Tales – Canis Major, tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
- Major/constell.html The Deep Photographic Guide to the Constellations: Canis Major[dead link]
Marejeo
- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 59 (online kwenye archive.org)
- Bond, Howard E.; Schaefer, Gail H.; Gilliland, Ronald L.; Holberg, Jay B.; Mason, Brian D.; Lindenblad, Irving W.; Seitz-Mcleese, Miranda; Arnett, W. David; Demarque, Pierre; Spada, Federico; Young, Patrick A.; Barstow, Martin A.; Burleigh, Matthew R.; Gudehus, Donald (2017). "The Sirius System and Its Astrophysical Puzzles: Hubble Space Telescope and Ground-based Astrometry". The Astrophysical Journal. 840 (2): 70, online hapa
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
- Lane, Edward William: Arabic-English Lexicon (London: Willams & Norgate 1863), Book I, Part 4 س - ص, uk. 1560, online hapa
- Liebert, J.; Young, P. A.; Arnett, D.; Holberg, J. B.; Williams, K. A. (2005). "The Age and Progenitor Mass of Sirius B". The Astrophysical Journal. 630 (1): L69–L72. online hapa