Andhra Pradesh

Andhra Pradesh (Telugu: ఆంధ్ర ప్రదేశ్, Kiurdu: آندھرا پردیش), ni moja kati ya majimbo 28 ya India. Jimbo lipo mjini kusini-mashariki mwa pwani ya India. Ni jimbo la nne kwa ukubwa wa eneo na ni la tano kwa hesabu ya wingi wa wakazi nchini India. Mji mkuu wake ni Hyderabad. Jumla ya pato la ndani ya Pradesh ni dola za Kimarekani zipatazi bilioni 100 na imeshika nafasi ya tatu miongoni mwa majimbo yote ya India.[1] Jimbo hili ni la pili kwa ukuwa na ukanda wa pwani ulio-mkubwa zaidi ambamo kuna km 972 (mi 604) miongoni mwa majimbo yote ya India.[2] Lugha ya kwanza mjini Andhra Pradesh ni Kitelugu na Kiurdu ni lugha rasmi katika baadhi ya sehemu,[3] wakati lugha zingine zinazozungumzwa mjini hapa ni pamoja na Kihindi, Kimarathi, Kitamil, Kannada, na Kioriya. Idadi ya wakazi wa mjini hapa ni 84,655,533 - kulingana na sensa ya mwaka wa 2011.

Moja ya mji ndani ya jimbo la wa Andhra Pradesh
Mahali pa Andhra Pradesh katika Uhindi
Ramani ya Andhra Pradesh

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Andhra Pradesh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.