Chad
Chad, kirasmi Jamhuri ya Chad (pia: Chadi), ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.
Jamhuri ya Chad | |
---|---|
جمهورية تشاد (Kiarabu) République du Tchad (Kifaransa) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unité, Travail, Progrès (Kifaransa) الاتحاد، العمل، التقدم (Kiarabu) "Umoja, Kazi, Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: La Tchadienne (Kifaransa) نشيد تشاد الوطني (Kiarabu) "Wimbo wa Chad" | |
Mahali pa Chad | |
Ramani ya Chad | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | N'Djamena |
Lugha rasmi | Kiarabu Kifaransa |
Makabila (asilimia)[1] | 26.6 Wasara 12.9 Waarabu 8.5 Wakanembu 7.2 Wamasalit 6.9 Watebu 4.8 Wamasana 3.7 Wabidiyo 3.7 Wabilala 3.0 Wamaba 2.6 Wadaju 2.5 Wamundang 2.4 Wagabri 2.4 Wazaghawa 2.1 Wafulani 2.0 Watupuri 1.6 Watama 1.4 Wakaro 1.3 Wabagirmi 1.0 Wamasmaje 2.6 Wachad wengine 0.7 Wageni |
Dini (asilimia)[2] | 55.1 Waislamu 41.1 Wakristo 2.4 Wakanamungu 1.3 dini asilia 0.1 wengine |
Serikali | Jamhuri yenye baraza la majeshi |
• Rais wa muda • Makamu wa Rais • Waziri Mkuu | Mahamat Déby Djimadoum Tiraina Succès Masra |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 1 284 000[3] |
• Maji (asilimia) | 1.9[3] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 18 523 165[3] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 12.596[4] |
• Kwa kila mtu | USD 702[4] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 32.375[4] |
• Kwa kila mtu | USD 1 806[4] |
Maendeleo (2022) | 0.394[5] - duni |
Jiografia
Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .
Kaskazini kuna milima ya Tibesti.
Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.
Historia
Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo.
Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.
Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.
Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.
Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.
Watu
Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018.
Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:
- Kaskazini wako hasa watu walioathiriwa sana na utamaduni wa Uislamu (55% za wakazi wote[6], wengi wakiwa Wasuni[7]). Mifano ni Waarabu (12.3%), Wafulbe, Wahaussa, Wazaghawa na wengineo. Wengi wao walikuwa wafugaji na sehemu ya makabila inaendelea hadi leo maisha ya kuhamahama.
- Kusini wako hasa watu wanaofuata Ukristo (41%, Wakatoliki wakiwa wengi kidogo kuliko Waprotestanti[8]) au dini asilia za Kiafrika (1%) kama Wasara (27.7%). Wengi wao hulima.
Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile[9].
Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa.
Tazama pia
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
- Vya serikali
- (Kifaransa) Serikali ya Chad Archived 4 Januari 2014 at the Wayback Machine.
- (Kifaransa) Official presidency site Archived 26 Februari 2011 at the Wayback Machine.
- Chief of State and Cabinet Members Archived 27 Julai 2009 at the Wayback Machine.
- Vingine
- Chad entry at The World Factbook
- Chad country study from Library of Congress
- Chad katika Open Directory Project
- Chad profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Chad
- Key Development Forecasts for Chad from International Futures
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |