Guinea Bisau


Gine-Bisau (Kiingereza: Guinea-Bissau) ni nchi ndogo katika Afrika ya Magharibi.

Jamhuri ya Gine-Bisau
República da Guiné-Bissau (Kireno)
𞤘𞤭𞤲𞤫 𞤄𞤭𞤧𞤢𞥄𞤱𞤮 (Kifulani)
ߖߌߣߍ ߺ ߓߌߛߊߥߏ߫ (Kimandinka)
Bendera ya Guinea Bisau
Bendera
Nembo ya Guinea Bisau
Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Unidade, Luta, Progresso (Kireno)
"Umoja, Harakati, Maendeleo"
Wimbo wa taifa:
Esta É a Nossa Pátria Bem Amada
"Hii ni Nchi Yetu Inayopendwa Sana"
Mahali pa Guinea Bisau
Mahali pa Guinea Bisau
Ramani ya Guinea Bisau
Ramani ya Guinea Bisau
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Bisau
11°52′ N 15°36′ W
Lugha rasmiKireno

Iko mwambaoni kwa Bahari Atlantiki ikipakana na Senegal upande wa kaskazini na Guinea upande wa kusini.

Jiografia

Guinea-Bisau ni kati ya nchi ndogo sana za Afrika ikiwa na eneo la kilomita mraba 36,125; takriban 22% ni visiwa na bahari. Sehemu ya bara ni tambarare. Funguvisiwa la Bissagos lenye visiwa 77 liko karibu na pwani.

Miji

Miji mikubwa zaidi ya Guinea Bisau ni: Bisau (wakazi 492,004), Gabú (wakazi 48,670), Bafatá (wakazi 37,875), Bissorã (wakazi 29,468), Bolama (wakazi 16,216) na Cacheu (14,320).

Historia

Zamani ilikuwa koloni la Ureno kwa jina la Guinea ya Kireno.

Baada ya uhuru (1973/1974) jina la mji mkuu wake lilishika nafasi ya nchi tawala kuwa Guinea-Bisau kwa kusudi la kuitofautisha na nchi jirani ya Guinea na ile ya Guinea ya Ikweta.

Watu

Wakazi walikuwa 1,515,000 mwaka 2010, wakati walikuwa 518,000 tu mwaka 1950.

Makabila

Waafrika ni 99%: makabila makubwa ni Wabalanta 30%, Wafulbe 30%, Wamanjaca 14%, Wamandinka 13%, Wapapel 7%). Wazungu na machotara ni chini ya 1%.

Lugha

Pamoja na lugha asilia, 32.1% za wakazi wanasema Kireno ambacho ndicho lugha rasmi na 90.4% wanatumia Krioli maalumu ya Kireno ambayo ni kama lugha ya taifa inayounganisha makabila. Lugha nyingine za kigeni zinazotumika ni Kifaransa (7%), Kiingereza (2.9%) na Kihispania (0.5%)

Dini

Takriban 46.1% ni Waislamu (hasa Wasuni), 30.6% wafuasi wa dini asilia za Kiafrika, 18.9% Wakristo (hasa Wakatoliki).

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Serikali
Biashara
Habari
Afya
Jiografia


Nchi za Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guinea Bisau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.