Kobalti


Kobalti (kutoka Kiingereza cobalt inayotoka Kijerumani kobalt) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi mpito yenye kifupi cha Co na namba atomia 27 katika mfumo radidia yenye uzani atomia 58.933.

Kobalti
Kobalti
Kobalti
Jina la ElementiKobalti
AlamaCo
Namba atomia27
Mfululizo safuMetali
Uzani atomia 58.933
Valensi2, 8, 15, 2
Densiti8.90 g/cm³
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka1768 K (1495 °C)
Kiwango cha kuchemka3200 K (2927 °C)
Asilimia za ganda la dunia4.7 %
Hali maada mango

Kobalti hupatikana mara chache kama metali tupu lakini zaidi ndani ya mitapo hasa za nikeli na shaba.

Tangu kale kampaundi zake hutumiwa kwa rangi na wino mbalimbali, hasa za buluu, kijani na njano. Kampaundi ya CoAl2O4 inatumiwa kutengeneza kioo cha buluu.

Katika karne ya 20 matumizi yalienea katika uzalishaji wa feleji, aloi yake inaongeza ugumu wa feleji.

Tangu kupatikana kwa simu za mkononi na magari ya umeme kobalti imekuwa muhimu sana kwa uzalishaji wa beteri. Hii ilisababisha mlipuko wa soko la kobalti na uchimbaji wake. Mwaka 2016 takriban asilimia 60 za mahitaji yote yalichimmbwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo[1].

Uchimbaji wa kobalti Duniani, nchi kwa nchi (tani)
Land2006[2]2013[3]2016[4]
Australia600064005100
Brazil100030005800
China140072007700
JD Kongo220005400066000
Kanada560069207300
Kuba400042004200
Moroko15001700
Kaledonia Mpya110031903300
Ufilipino30003500
Urusi510063006200
Zambia860052004600
Afrika Kusini30003000
nchi nyingine za Dunia120080008300
Jumla57.500110.000123.000

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kobalti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.