Volodymyr Zelensky

Rais wa Ukraine.


Volodymyr Oleksandrovych Zelensky (alizaliwa 25 Januari 1978) ni mwanasiasa, mwandishi na mwigizaji wa filamu, mchekeshaji na rais wa sasa (wa 6) wa Ukraine toka 20 Mei 2019.

Volodymyr Zelensky
Zelensky wakati wa sherehe ya kuapishwa.
Zelensky wakati wa sherehe ya kuapishwa.
Rais
Tarehe ya kuzaliwa 25 Januari 1978
Kazimwanasiasa, mwandishi na mwigizaji wa filamu, mchekeshaji na rais

Utoto na elimu

Volodymyr Zelenskyy alizaliwa katika familia ya Kiyahudi katika mji wa Kryvyi Rih, wakati ule sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamaa ya Ukraine.[1][2][3][4] Lugha yake ya kwanza ni Kirusi[5].

Baba yake Oleksandr Zelenskyy alikuwa profesa wa sayansi za kompyuta, mama yake alikuwa mhandisi.[6][7][8] Babu wa Zelensky alikuwa mwanajeshi katika Jeshi Jekundu la Kisovyeti wakazi wa Vita Kuu ya Pili akafikia cheo cha kanali.[9] Ndugu kadhaa wa familia waliuawa na Wajerumani kwa sababu ya kuwa Wayahudi katika Maangamizi Makuu ya Wayahudi.[10] Volodymyr aliendelea kusoma sheria lakini hakufanya kazi ya wakili baada ya kuhitimu.[2]

Mwigizaji na mtayarishaji

Tangu alipokuwa mwanafunzi alitumia nafasi nyingi ya kazi ya mwigizaji. Mwaka 1997 aliunda kundi la waigizaji wachechi la Kvartal 95.[11][12] Kuanzia mwaka 2003 kundi hilo lilitayarisha video kwa ajili ya runinga ya kitaifa ya Ukraine.[13]

Kati ya miaka 2015-2019, Kvartal 95 ilirusha mfululizo wa vipindi vya televisheni vilivyoitwa Servant of the People ambapo Zelensky aliigiza kama Rais wa Ukraine. Chama cha siasa Servant of the People kilianzishwa na wafanyakazi wa Kvartal 95 mnamo Machi 2018.[14][15]

Siasa

Tarehe 31 Desemba 2018, Zelensky alitangaza rasmi kuwa atagombea urais.[16] Miezi sita kabla ya kutangaza nia yake hiyo, alikuwa tayari kati ya wagombea waliokuwa wakiongoza kwenye kura za maoni.[17][15] Zelensky alipata asilimia 30 za kura kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Akaingia katika awamu ya pili pamoja na rais mtendaji Petro Poroshenko akashinda kwa kupata asilimia 72.33.[18]

Filamu

MwakaJinaNafasi
2009Love in the Big CityIgor
2011Office Romance. Our TimeAnatoly Efremovich Novoseltsev
2012Love in the Big City 2Igor
2012Rzhevsky Versus NapoleonNapoleon
20128 First DatesNikita Sokolov
2014Love in VegasI gor Zelensky
20158 New DatesNikita Andreevich Sokolov

Televisheni

MwakaJinaNafasiNotes
2006Dancing with the Starsmshindani
2008–2012Svatymtayarishaji
2015–2019Servant of the PeopleVasyl Petrovych Holoborodko, mwalimu wa historia/Rais wa Ukraine

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Volodymyr Zelensky kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.