Amazonas (mto)

Mto Amazonas (kwa Kireno: Rio Amazonas) ndio mto mkubwa kuliko yote duniani. Unabeba maji zaidi kuliko mito ya Nile, Mississippi na Yangtse kwa pamoja.

Mto Amazonas ni mto mkubwa kuliko mito yote duniani


Mto wa Amazonas
Beseni ya Amazonas
Chanzomlima Nevado Mismi (Peru)
MdomoAtlantiki
NchiBrazil (62.4%), Peru (16.3%)
Bolivia (12.0%), Kolombia (6.3%)
Ekuador (2.1%)
Urefu6,400 km
Kimo cha chanzotakriban 5,597 m
Tawimito upande wa kuliaPurus, Madeira, Tapajós, Xingu, Tocantins
Tawimito upande wa kushotoMarañón, Japurá, Rio Negro
Mkondo219,000 m³/s
Eneo la beseni6,915,000 km²
Miji mikubwa kando lakeManaus, Macapa, Santarem

Una chanzo chake katika milima ya Andes inavuka beseni lake hadi Atlantiki kupitia eneo kubwa la misitu minene. Sehemu kubwa ya mwendo wake iko katika nchi ya Brazil.

Kuhusu urefu hakuna bado mapatano ya kitaalamu kama Nile au Amazonas ndio mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto lipi lenye chanzo cha mbali zaidi linaokubaliwa na wataalamu. Mwaka 1969 urefu wake ulipimwa kuwa km 6.400.

Amazonas ina matawimto zaidi ya 10,000 na kati ya hayo 17 yana urefu wa zaidi ya km 1,600 yakishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu.

Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufikia hadi 100 wakati wa mafuriko ya kila mwaka. Delta ya Amazonas ina upana wa kilomita mia kadhaa; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la km² 49,000 ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi.

Amazonas ni njia muhimu ya mawasiliano na usafiri nchini Brazil. Meli kubwa za baharini zinaweza kuingia hadi bandari ya Manaus iliyoko km 800 ndani ya bara. Meli ndogo za baharini hadi uzito wa tani 3,000 zinaweza kuvuka Brazil yote hadi kufika Peru.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Amazonas (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.