Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mtendaji mkuu wa UM na mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya UM ambayo ni kati ya vitengo muhimu vya Umoja wa Mataifa.

Uteuzi wa Katibu Mkuu

Katibu Mkuu huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kwa muda wa miaka mitano. Jina linapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama la UM. Kwa hiyo uteuzi wa Katibu Mkuu uko mkononi mwa Baraza la Usalama na kila taifa mjumbe wa kudumu linaweza kuzuia jina fulani lisipelekwa kwa njia ya Veto yake. Lakini Baraza la Usalama linapaswa kumteua mtu atakayepata kura za kutosha katika Mkutano Mkuu.

Hakuna sheria juu ya muda wa kazi yake lakini hadi sasa hakuna Katibu Mkuu aliyehudumia UM zaidi ya vipindi viwili au miaka 10. Kuna kawaida ya kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inapita kwenye mabara yote ingawa hiyo si sheria.

Mshahara wa Katibu Mkuu ni dolar za Marekani 176,877 kwa mwaka. (2006).

Orodha ya Makatibu Wakuu

#PichaJina
Muda wa ukatibu wake
Taifa lakeMengineyoViungo
  Gladwyn Jebb24 Oktoba 1945 –
2 Februari 1946
Uingerezakaimu Katibu Mkuu 
1 Trygve Halvdan Lie2 Februari 1946 –
10 Novemba 1952
NorweialijiuzuluBiografia
2Faili:Dag Hammarskjold.jpgDag Hammarskjöld10 Aprili 1953 –
18 Septemba 1961
Uswidialikufa katika ajali ya ndege yake huko Rhodesia ya Kaskazini (leo Zambia)Biografia
3 Sithu U Thant3 Novemba 1961 –
31 Desemba 1971
Burma (leo Myanmar)kazi ya tar. 3 Novemba 1961 hadi 30 Novemba 1962 kaimu Katibu MkuuBiografia
4 Kurt Waldheim1 Januari 1972 –
31 Desemba 1981
AustriaVeto ya China ilizuia kipindi cha tatuBiografia
5 Javier Pérez de Cuéllar1 Januari 1982 –
31 Desemba 1991
Peruhakugombea mara ya tatuBiografia
6 Boutros Boutros-Ghali1 Januari 1992 –
31 Desemba 1996
MisriVeto ya Marekani ilizuia kipindi cha piliBiografia
7 Kofi Annan1 Januari 1997 –
31 Desemba 2006
Ghanahakugombea kipindi cha tatuBiografia
8 Ban Ki-moon1 Januari 2007 –Korea KusiniBiografia

Makamu wa Katibu Mkuu

Mkutano Mkuu uliamua 1997 kuanzisha cheo kipya cha makamu wa Katibu Mkuu.

Tangu 7 Januari 2007 Asha-Rose Migiro kutoka Tanzania amepewa nafasi hii. Alimfuata Mark Malloch Brown.


Viungo vya Nje