Latvia
Latvia (kwa Kilatvia: Latvija au Latvijas Republika, kwa Kilivonia: Lețmō au Leţmō Vabāmō) ni nchi ya Kibalti katika Ulaya ya Kaskazini.
Latvia |
---|
Imepakana na Estonia, Lithuania, Belarus na Urusi. Uswidi iko ng'ambo ya bahari ya Baltiki.
Latvia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1 Mei 2004.
Historia
Kwa muda mrefu Estonia ilikuwa chini ya Wajerumani, Wapolandi na Waswidi, halafu (1710) sehemu ya Dola la Urusi.
Katika miaka 1918-1940 ilikuwa jamhuri halafu miaka 1940-1991 mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.
Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Latvia ilijitangaza nchi huru tena.
Latvia ilijiunga na Umoja wa Ulaya baada ya azimio la Halmashauri Kuu ya Ulaya ya tarehe 13 Desemba 2002 iliyokutana Kopenhagen.
Katika kura ya maoni ya tarehe 20 Septemba 2003 ni 66.9% za Walatvia wote waliokubali azimio hilo.
Latvia iliingia rasmi katika Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004 pamoja na nchi nyingine 9 za Ulaya mashariki.
Watu
Idadi ya watu inapungua, na sasa iko chini ya milioni 2.
Wakazi wengi ni Walatvia 61.6%, halafu Warusi 25.8%, Wabelarus 3,4%, Waukraina 2,3%, Wapolandi 2,1%, Walituania 1.2% na wengine 4.8%.
Lugha rasmi ni Kilatvia, ambayo ni mojawapo ya lugha za Kibalti. Wananchi walipiga kura ya kukataa Kirusi kama lugha rasmi ya pili.
Upande wa dini, wengi (78.5%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, ingawa 7% tu wanashiriki ibada mara kwa mara. Hasa ni Walutheri (34.2%), Wakatoliki (24.1%) na Waorthodoksi (19.4%). Asilimia 21.1 hawana dini yoyote.
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
- Rīga Wiki Archived 6 Julai 2005 at the Wayback Machine.
Angalia mengine kuhusu Latvia kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
- Serikali
- President of Latvia
- Parliament of Latvia
- Government of Latvia
- Ministry of Foreign Affairs of Latvia
- Statistical Office of Latvia
- Latvian Institute
- Bank of Latvia
- Taarifa za jumla
- Latvia Online
- European Union country profile
- Britannica Online Encyclopedia
- BBC News country profile
- Latvia entry at The World Factbook
- Latvia Archived 11 Oktoba 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Latvia katika Open Directory Project
- Key Development Forecasts for Latvia from International Futures
- Elimu na utamaduni
- Latvian Cultural Canon
- Latvian Culture Map
- Latvian Culture Portal Archived 18 Januari 2013 at the Wayback Machine.
- Latvian Community Archived 3 Februari 2016 at the Wayback Machine.
- Livonian Culture Portal
- State Agency of Cultural Heritage
- National Library of Latvia Archived 1 Juni 2021 at the Wayback Machine.
- Latvian Heritage
- Latvian Music Information Centre
- Utalii
- Ramani
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Latvia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |