Gesi asilia

Gesi asilia ni gesi inayopatikana katika ardhi na inayotumiwa na binadamu kama fueli.

Uzalishaji wa gesi asilia duniani

Tabia za gesi asilia

Kikemia ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali kama methani zilizotokana na kuoza kwa mata ogania kama mimea ya miaka mingi iliyopita.

Gesi asilia inapatikana katika ardhi yenye mwamba wenye vinyweleo vingi ulioko chini ya ganda la mwamba imara zaidi unaozuia gesi kupanda juu zaidi.

Ni fueli kisukuu ambayo ni muhimu kwa matumizi ya kibinadamu katika injini za kutengeneza umeme na pia kwa kuongeza joto katika nyumba za watu kwenye nchi zenye baridi.

Kwa matumizi ya kibinadamu gesi asilia hukamatwa kwenye chanzo chake. Baadaye inasafishwa kwa kuondoa maji na hidrokaboni mbalimbali ili kufikia kiwango cha juu cha methani cha asilimia 90 na zaidi[1]. Baada ya kusafishwa inafaa kusafirishwa katika mabomba kwa kilomita mamia au maelfu hadi pale inapogawiwa kwa watumiaji.

Kama hakuna mabomba pale gesi inapozalishwa gesi inabadilishwa kuwa gesi miminika, kwa kuipoza hadi sentigredi -161°C (chini ya sifuri). Katika hali hiyo gesi ni miminika inachukua nafasi ndogo tu. Husafirishwa kwa meli zinazobeba tangi zinazopoozwa na kupokewa katika bandari maalumu zenye vifaa vya kutunzia gesi hii baridi.

Chanzo cha gesi na petroliamu

(linganisha: Chanzo cha mafuta ya petroli)

Mara nyingi gesi asilia hutokea mahali pamoja na mafuta ya petroli (petroliamu) kwa sababu dutu hizo mbili zilitokea pamoja kwenye tako la bahari kutokana na viumbe vya algae na planktoni.

Bahari imejaa viumbe vidogo hivi ambavyo vinashuka chini hadi tako la bahari baada ya kufa. Huko haviweza kuoza kama kawaida kutokana na ukosefu wa oksijeni, hivyo hubadilika kuwa ganda la tope ogania. Baada ya miaka milioni ganda la tope hufunikwa na mashapo kama mchanga utakaokuwa mwamba. Chini ya funiko hilo tope ogania hupokea shinikizo kubwa pia joto na hivyo molekuli zinazojenga mwili wa algae hupasuliwa kuwa safu za hidrokaboni. Zile zilizo nzito zinakaa chini kama mafuta na sehemu nyepesi zinapanda juu ya mafuta kama gesi. Hapo gesi inashikwa na tabaka la mwamba imara linalozuia kupanda kwake. Kama tabaka la namna hiyo halipo hakuna gesi tena maana yote imeshapotea kwa kupanda juu na kuingia hewani muda mrefu uliopita.

Kikemia mafuta yale sawa na gesi asilia ni hasa mchanganyiko wa hidrokaboni mbalimbali lakini gesi huwa na molekuli nyepesinyepesi tofauti na mafuta yenye molekuli nzitonzito.

Chini ya ardhi gesi ambayo ni nyepesi hupatikana juu ya mafuta. Wakati akiba ya gesi na petroliamu chini ya ardhi hutobolewa kwa keekee gesi inatangulia kuondoka. Zamani makampuni yaliyotafuta petroliamu yalichoma gesi bila kuitumia lakini siku hizi thamani kubwa ya gesi imetambuliwa.

Gesi asilia inasafirishwa kutoka mahali inapopatikana ama kwa meli za pekee au kwa mabomba makubwa ya kimataifa.

Uzalishaji

Mnamo mwaka 2004 takriban mita za mjao bilioni 589 zilizalishwa. Zilitosheleza asilimia 24 za mahitaji ya nishati duniani. Nchi zinazozalisha gesi nyingi duniani kwa sasa ni Urusi na Marekani. Urusi ina pia akiba kubwa duniani maana kuna bado kiasi kikubwa sana ya gesi chini ya ardhi. Lakini nyingine zenye akiba kubwa ni nchi zilizopo kando ya Ghuba la Uajemi ambazo ni Uajemi, Qatar, Saudia na Falme za Kiarabu.

Gesi hukatamwa kwenye chanzo chake, kusafishwa halafu kusafirishwa kwa njia ya bomba hadi watumiaji au hadi bandari inapowekwa kwenye meli za tangi. Kwa kawaida gesi asilia ama hugandamizwa kuwa miminika kwa ajili ya usafirishaji kwenye mabomba.

NchiAkiba zilizothebitishwa
(millioni m³)
TareheUzalishaji
(million m³)
TareheMatumizi
(millioni m³)
Tarehemahuruji
(millioni m³)
Tarehemadhuhuli
(millioni m³)
Date
Dunia175,400,000
makadirio 20083,021,000
makadirio 20073,198,000
makadirio 2007929,900
makadirio 2007957,600
2007
Urusi44,650,000
Nafasi ya 1
makadirio 2008654,000
Nafasi ya 1
makadirio 2007481,000
Nafasi ya 2
makadirio 2007173,000
Nafasi ya 1
makadirio 200768,200
Nafasi ya 5
makadirio 2007
Uajemi26,850,000
Nafasi ya 2
makadirio 2008111,900
Nafasi ya 4
makadirio 2007111,800
Nafasi ya 3
makadirio 20076,200
Nafasi ya 25
makadirio 20076,100
Nafasi ya 27
makadirio 2007
Qatar25,630,000
Nafasi ya 3
makadirio 200859,800
Nafasi ya 14
makadirio 200720,500
Nafasi ya 33
makadirio 200739,300
Nafasi ya 7
makadirio 20070
makadirio 2007
Saudia7,167,000
Nafasi ya 4
makadirio 200875,900
Nafasi ya 8
makadirio 200775,900
Nafasi ya 9
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Falme za Kiarabu6,071,000
Nafasi ya 5
makadirio 200848,790
Nafasi ya 17
makadirio 200643,110
Nafasi ya 16
makadirio 20066,848
Nafasi ya 24
2005 est.1,343
Nafasi ya 46
2005
Marekani5,977,000
Nafasi ya 6
makadirio 2008593,400
Nafasi ya 1
2009 est.646,600
Nafasi ya 1
2009 est.23,280
Nafasi ya 10
makadirio 2007130,300
Nafasi ya 1
makadirio 2007
Nigeria5,210,000
Nafasi ya 7
makadirio 200834,100
Nafasi ya 22
makadirio 200712,900
Nafasi ya 41
makadirio 200721,200
Nafasi ya 11
makadirio 20070
makadirio 2007
Venezuela4,708,000
Nafasi ya 8
makadirio 200826,500
Nafasi ya 26
makadirio 200726,500
Nafasi ya 28
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Algeria4,502,000
Nafasi ya 9
makadirio 200885,700
Nafasi ya 6
makadirio 200726,300
Nafasi ya 29
makadirio 200759,400
Nafasi ya 4
makadirio 20070
makadirio 2007
Iraq3,170,000
Nafasi ya 10
makadirio 200815,660
Nafasi ya 32
makadirio 20089,454
Nafasi ya 46
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 2007
Kazakhstan2,832,000
Nafasi ya 11
makadirio 200827,880
Nafasi ya 25
makadirio 200730,580
Nafasi ya 26
makadirio 20078,100
Nafasi ya 23
makadirio 200710,800
Nafasi ya 17
makadirio 2007
Turkmenistan2,832,000
Nafasi ya 12
makadirio 200868,880
Nafasi ya 11
makadirio 200719,480
Nafasi ya 35
makadirio 200749,400
Nafasi ya 6
makadirio 20070
makadirio 2007
Indonesia2,659,000
Nafasi ya 13
makadirio 200856,000
Nafasi ya 15
makadirio 200723,400
Nafasi ya 30
makadirio 200732,600
Nafasi ya 8
makadirio 20070
makadirio 2007
Umoja wa Ulaya2,476,000
makadirio 2008197,800
makadirio 2007497,300
makadirio 2007NA
NANA
NA
Malaysia2,350,000
Nafasi ya 14
makadirio 200864,500
Nafasi ya 13
makadirio 200732,900
Nafasi ya 23
makadirio 200731,600
Nafasi ya 9
makadirio 20070
makadirio 2007
China2,265,000
Nafasi ya 15
makadirio 200869,270
Nafasi ya 10
makadirio 200770,510
Nafasi ya 10
makadirio 20075,360
Nafasi ya 26
makadirio 20073,871
Nafasi ya 34
makadirio 2007
Norwei2,241,000
Nafasi ya 16
makadirio 200899,300
Nafasi ya 5
makadirio 20086,500
Nafasi ya 52
makadirio 200785,700
Nafasi ya 3
makadirio 20070
makadirio 2007
Uzbekistan1,841,000
Nafasi ya 17
makadirio 200865,190
Nafasi ya 12
makadirio 200751,180
Nafasi ya 13
makadirio 200714,010
Nafasi ya 15
makadirio 20070
makadirio 2007
Misri1,656,000
Nafasi ya 18
makadirio 200847,500
Nafasi ya 18
makadirio 200731,800
Nafasi ya 24
makadirio 200715,700
Nafasi ya 14
makadirio 20070
makadirio 2007
Kanada1,648,000
Nafasi ya 19
makadirio 2008187,000
Nafasi ya 3
makadirio 200792,900
Nafasi ya 6
makadirio 2007107,300
Nafasi ya 2
makadirio 200713,200
Nafasi ya 15
makadirio 2007
Kuwait1,586,000
Nafasi ya 20
makadirio 200812,500
Nafasi ya 37
makadirio 200612,500
Nafasi ya 42
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Libya1,419,000
Nafasi ya 21
makadirio 200814,800
Nafasi ya 33
makadirio 20066,390
Nafasi ya 53
makadirio 20069,900
Nafasi ya 21
makadirio 20070
makadirio 2007
Uholanzi1,416,000
Nafasi ya 22
makadirio 200876,330
Nafasi ya 7
makadirio 200746,420
Nafasi ya 14
makadirio 200755,660
Nafasi ya 5
makadirio 200725,730
Nafasi ya 12
makadirio 2007
Ukraine1,104,000
Nafasi ya 23
makadirio 200821,050
Nafasi ya 29
makadirio 200866,320
Nafasi ya 12
makadirio 20084,000
Nafasi ya 28
makadirio 200665,400
Nafasi ya 6
makadirio 2007
Uhindi1,075,000
Nafasi ya 24
makadirio 200831,700
Nafasi ya 23
makadirio 200741,700
Nafasi ya 18
makadirio 20070
makadirio 200710,000
Nafasi ya 21
makadirio 2007
Azerbaijan849,500
Nafasi ya 25
makadirio 20089,770
Nafasi ya 41
makadirio 20079,770
Nafasi ya 45
makadirio 20070
makadirio 20070
2005
Australia849,500
Nafasi ya 26
makadirio 200843,620
Nafasi ya 20
makadirio 200729,400
Nafasi ya 27
makadirio 200719,910
Nafasi ya 12
makadirio 20075,689
Nafasi ya 28
makadirio 2007
Oman849,500
Nafasi ya 27
makadirio 200824,100
Nafasi ya 28
makadirio 200711,000
Nafasi ya 44
makadirio 200713,100
Nafasi ya 16
makadirio 20070
makadirio 2007
Pakistan792,800
Nafasi ya 28
makadirio 200830,800
Nafasi ya 24
makadirio 200730,800
Nafasi ya 25
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Bolivia750,400
Nafasi ya 29
makadirio 200814,700
Nafasi ya 34
makadirio 20073,000
Nafasi ya 71
makadirio 200711,700
Nafasi ya 18
makadirio 20070
makadirio 2007
Trinidad na Tobago481,300
Nafasi ya 30
makadirio 200839,000
Nafasi ya 21
makadirio 200720,800
Nafasi ya 32
makadirio 200718,100
Nafasi ya 13
makadirio 20070
makadirio 2007
Yemen478,500
Nafasi ya 31
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Argentina446,000
Nafasi ya 32
makadirio 200844,800
Nafasi ya 19
makadirio 200744,100
Nafasi ya 15
makadirio 20072,600
Nafasi ya 31
makadirio 20071,900
Nafasi ya 44
makadirio 2007
Ufalme wa Maungano (Uingereza)412,000
Nafasi ya 33
makadirio 200872,300
Nafasi ya 9
makadirio 200791,100
Nafasi ya 7
makadirio 200710,400
Nafasi ya 19
makadirio 200729,200
Nafasi ya 11
makadirio 2007
Meksiko392,200
Nafasi ya 34
makadirio 200855,980
Nafasi ya 16
makadirio 200768,290
Nafasi ya 11
makadirio 20072,973
Nafasi ya 29
makadirio 200711,690
Nafasi ya 16
makadirio 2007
Brunei390,800
Nafasi ya 35
makadirio 200813,800
Nafasi ya 35
makadirio 20063,990
Nafasi ya 62
makadirio 20069,400
Nafasi ya 22
makadirio 20070
makadirio 2007
Brazil347,700
Nafasi ya 36
makadirio 20089,800
Nafasi ya 40
makadirio 200719,800
Nafasi ya 34
makadirio 20070
makadirio 200710,000
Nafasi ya 20
makadirio 2007
Peru334,700
Nafasi ya 37
makadirio 20083,400
Nafasi ya 50
makadirio 20083,400
Nafasi ya 67
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 2008
Thailand331,200
Nafasi ya 38
makadirio 200825,400
Nafasi ya 27
makadirio 200735,300
Nafasi ya 21
makadirio 20070
makadirio 20079,800
Nafasi ya 22
makadirio 2007
Burma283,200
Nafasi ya 39
makadirio 200812,600
Nafasi ya 36
makadirio 20063,620
Nafasi ya 64
makadirio 20069,900
Nafasi ya 20
makadirio 20070
makadirio 2007
Angola269,800
Nafasi ya 40
makadirio 2008680
Nafasi ya 65
makadirio 2006680
Nafasi ya 90
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Ujerumani254,800
Nafasi ya 41
makadirio 200817,960
Nafasi ya 30
makadirio 200797,440
Nafasi ya 5
makadirio 200712,220
Nafasi ya 17
makadirio 200788,350
Nafasi ya 3
makadirio 2007
Syria240,700
Nafasi ya 42
makadirio 20086,500
Nafasi ya 46
makadirio 20084,400
Nafasi ya 58
makadirio 2008NA
NA0
makadirio 2007
Papua Guinea Mpya226,500
Nafasi ya 43
makadirio 2008140
Nafasi ya 75
makadirio 2006140
Nafasi ya 97
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Timor-Leste200,000
Nafasi ya 44
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Vietnam192,500
Nafasi ya 45
makadirio 20086,860
Nafasi ya 45
makadirio 20076,860
Nafasi ya 50
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Poland164,800
Nafasi ya 46
makadirio 20086,025
Nafasi ya 47
makadirio 200716,380
Nafasi ya 38
makadirio 200745
Nafasi ya 38
makadirio 200710,120
Nafasi ya 19
makadirio 2007
Bangladesh141,600
Nafasi ya 47
makadirio 200815,700
Nafasi ya 31
makadirio 200715,700
Nafasi ya 39
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Cameroon135,100
Nafasi ya 48
makadirio 200820
Nafasi ya 86
makadirio 200620
Nafasi ya 106
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Msumbiji127,400
Nafasi ya 49
makadirio 20081,650
Nafasi ya 59
makadirio 20061,450
Nafasi ya 81
makadirio 20060
2005 est.0
makadirio 2007
Colombia122,900
Nafasi ya 50
makadirio 20087,220
Nafasi ya 44
makadirio 20067,220
Nafasi ya 49
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Ufilipino98,540
Nafasi ya 51
makadirio 20082,200
Nafasi ya 56
makadirio 20062,200
Nafasi ya 77
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Chile97,970
Nafasi ya 52
makadirio 20081,800
Nafasi ya 58
makadirio 20074,200
Nafasi ya 59
makadirio 20070
makadirio 20072,400
Nafasi ya 39
makadirio 2007
Italia94,150
Nafasi ya 53
makadirio 20089,706
Nafasi ya 42
makadirio 200784,890
Nafasi ya 8
makadirio 200768
Nafasi ya 37
makadirio 200773,950
Nafasi ya 4
makadirio 2007
Bahrain92,030
Nafasi ya 54
makadirio 200811,330
Nafasi ya 39
makadirio 200611,330
Nafasi ya 43
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Jamhuri ya Kongo90,610
Nafasi ya 55
makadirio 2008180
Nafasi ya 71
makadirio 2006180
Nafasi ya 95
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Sudan84,950
Nafasi ya 56
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Kuba70,790
Nafasi ya 57
makadirio 20081,218
Nafasi ya 62
20071,218
Nafasi ya 85
20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Denmark70,510
Nafasi ya 58
makadirio 20089,223
Nafasi ya 43
makadirio 20074,555
Nafasi ya 57
makadirio 20074,517
Nafasi ya 27
makadirio 20070
makadirio 2007
Tunisia65,130
Nafasi ya 59
makadirio 20082,550
Nafasi ya 53
makadirio 20063,850
Nafasi ya 63
makadirio 20060
makadirio 20070
2005
Romania63,000
Nafasi ya 60
makadirio 200812,500
Nafasi ya 38
makadirio 200617,090
Nafasi ya 37
20070
makadirio 20074,800
Nafasi ya 29
makadirio 2007
Namibia62,290
Nafasi ya 61
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Rwanda56,630
Nafasi ya 62
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Korea Kusini50,000
Nafasi ya 63
makadirio 2008640
Nafasi ya 67
makadirio 200737,000
Nafasi ya 19
makadirio 20070
makadirio 200734,400
Nafasi ya 10
makadirio 2007
Afghanistan49,550
Nafasi ya 64
makadirio 200820
Nafasi ya 85
makadirio 200620
Nafasi ya 105
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Serbia48,140
Nafasi ya 65
makadirio 2008650
Nafasi ya 66
2005 est.2,550
Nafasi ya 72
2005 est.0
2005 est.2,100
Nafasi ya 41
2004 est.
Kroatia40,900
Nafasi ya 66
makadirio 20082,892
Nafasi ya 52
20073,300
Nafasi ya 68
2007751.7
Nafasi ya 33
20071,055
Nafasi ya 49
2007
Guinea ya Ikweta36,810
Nafasi ya 67
makadirio 20081,300
Nafasi ya 60
makadirio 20061,300
Nafasi ya 83
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Israel30,440
Nafasi ya 68
makadirio 20082,350
Nafasi ya 55
makadirio 20062,270
Nafasi ya 74
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
New Zealand29,670
Nafasi ya 69
makadirio 20084,573
Nafasi ya 48
makadirio 20074,572
Nafasi ya 56
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Gabon28,320
Nafasi ya 70
makadirio 2008100
Nafasi ya 77
makadirio 2006100
Nafasi ya 99
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Mauritania28,320
Nafasi ya 71
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Cote d'Ivoire28,320
Nafasi ya 72
makadirio 20081,300
Nafasi ya 61
makadirio 20061,300
Nafasi ya 84
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Ethiopia24,920
Nafasi ya 73
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Ghana22,650
Nafasi ya 74
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Japan20,900
Nafasi ya 75
makadirio 20083,729
Nafasi ya 49
makadirio 2007100,300
Nafasi ya 4
makadirio 20070
makadirio 200795,620
Nafasi ya 2
makadirio 2007
Austria16,140
Nafasi ya 76
makadirio 20081,848
Nafasi ya 57
makadirio 20078,436
Nafasi ya 48
makadirio 20072,767
Nafasi ya 30
makadirio 20079,658
Nafasi ya 23
makadirio 2007
Slovakia14,160
Nafasi ya 77
makadirio 2008128
Nafasi ya 76
makadirio 20076,216
Nafasi ya 54
makadirio 2007180
Nafasi ya 35
makadirio 20076,268
Nafasi ya 26
makadirio 2007
Ireland9,911
Nafasi ya 78
makadirio 2008457
Nafasi ya 68
makadirio 20074,984
Nafasi ya 55
makadirio 20070
makadirio 20074,552
Nafasi ya 31
makadirio 2007
Ecuador9,369
Nafasi ya 79
makadirio 2006280
Nafasi ya 70
makadirio 2006280
Nafasi ya 93
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Georgia8,495
Nafasi ya 80
makadirio 200810
Nafasi ya 89
makadirio 20071,490
Nafasi ya 80
makadirio 20070
makadirio 20071,480
Nafasi ya 45
makadirio 2007
Uturuki8,495
Nafasi ya 81
makadirio 2008893
Nafasi ya 64
makadirio 200736,600
Nafasi ya 20
makadirio 200731
Nafasi ya 39
makadirio 200735,830
Nafasi ya 8
makadirio 2007
Hungaria8,098
Nafasi ya 82
makadirio 20082,545
Nafasi ya 54
makadirio 200713,360
Nafasi ya 40
makadirio 2007138
Nafasi ya 36
makadirio 200710,450
Nafasi ya 18
makadirio 2007
France7,277
Nafasi ya 83
makadirio 2008953
Nafasi ya 63
makadirio 200742,690
Nafasi ya 17
makadirio 2007966
Nafasi ya 32
makadirio 200742,900
Nafasi ya 7
makadirio 2007
Tanzania6,513
Nafasi ya 84
makadirio 2008146
Nafasi ya 74
makadirio 2006146
Nafasi ya 96
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Taiwan6,229
2008416
200713,600
20070
makadirio 200810,900
2007
Jordan6,031
Nafasi ya 85
makadirio 2008320
Nafasi ya 69
makadirio 20062,250
Nafasi ya 76
makadirio 20060
makadirio 20072,400
Nafasi ya 40
makadirio 2007
Bulgaria5,663
Nafasi ya 86
makadirio 20080
makadirio 20073,500
Nafasi ya 65
makadirio 20070
20073,229
Nafasi ya 37
2007
Somalia5,663
Nafasi ya 87
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Tajikistan5,663
Nafasi ya 88
makadirio 200816
Nafasi ya 88
2008542.7
Nafasi ya 91
20080
2008512.7
Nafasi ya 53
2008
Kyrgyzstan5,663
Nafasi ya 89
makadirio 200818
Nafasi ya 87
makadirio 2007768
Nafasi ya 89
makadirio 20070
makadirio 2007750
Nafasi ya 52
makadirio 2007
Ucheki3,964
Nafasi ya 90
makadirio 2008172
Nafasi ya 72
makadirio 20078,622
Nafasi ya 47
makadirio 2007402
Nafasi ya 34
makadirio 20078,628
Nafasi ya 24
makadirio 2007
Guatemala2,960
Nafasi ya 91
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Belarus2,832
Nafasi ya 92
makadirio 2008164
Nafasi ya 73
makadirio 200721,760
Nafasi ya 31
makadirio 20070
makadirio 200721,600
Nafasi ya 13
makadirio 2007
Hispania2,548
Nafasi ya 93
makadirio 200888
Nafasi ya 78
makadirio 200734,430
Nafasi ya 22
makadirio 20070
makadirio 200734,470
Nafasi ya 9
makadirio 2007
Ugiriki1,982
Nafasi ya 94
makadirio 200824
Nafasi ya 84
makadirio 20074,069
Nafasi ya 61
makadirio 20070
makadirio 20074,100
Nafasi ya 32
makadirio 2007
Moroko1,557
Nafasi ya 95
makadirio 200860
Nafasi ya 79
makadirio 200660
Nafasi ya 101
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Benin1,133
Nafasi ya 96
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo991.1
Nafasi ya 97
makadirio 20080
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Albania849.5
Nafasi ya 98
makadirio 200830
Nafasi ya 82
makadirio 200630
Nafasi ya 103
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Barbados141.6
Nafasi ya 99
makadirio 200829.17
Nafasi ya 83
makadirio 200629.17
Nafasi ya 104
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007
Afrika Kusini27.16
Nafasi ya 100
makadirio 20062,900
Nafasi ya 51
makadirio 20063,100
Nafasi ya 70
makadirio 20060
makadirio 20070
2005
Macau0.3
makadirio 20080
makadirio 200881.6
makadirio 20080
makadirio 200881.9
makadirio 2008
Aruba0
20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Botswana0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Ubelgiji0
20060
makadirio 200717,390
Nafasi ya 36
makadirio 20070
makadirio 200717,340
Nafasi ya 14
makadirio 2007
Visiwa vya Solomon0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Morisi0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Mali0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Masedonia0
makadirio 20080
makadirio 2007100
Nafasi ya 100
makadirio 20060
makadirio 2007102.8
Nafasi ya 56
2007
Malawi0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Montserrat0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Mongolia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Moldova0
makadirio 200650
Nafasi ya 80
makadirio 20062,440
Nafasi ya 73
makadirio 20070
makadirio 20072,440
Nafasi ya 38
makadirio 2007
Madagaska0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Lithuania0
makadirio 20060
makadirio 20073,440
Nafasi ya 66
makadirio 20070
makadirio 20073,440
Nafasi ya 35
makadirio 2007
Zimbabwe0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Zambia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Eswatini0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Samoa0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Sahara ya Magharibi0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
U.S. Virgin Islands0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
British Virgin Islands0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Saint Vincent na Grenadini0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Uruguay0
makadirio 20060
makadirio 2007102.8
Nafasi ya 98
makadirio 20070
makadirio 2007116.9
Nafasi ya 55
2007
Burkina Faso0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Uganda0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Sao Tome na Principe0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Togo0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Tonga0
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Visiwa vya Turks na Caicos0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Uswisi0
makadirio 20060
makadirio 20073,232
Nafasi ya 69
makadirio 20070
makadirio 20073,232
Nafasi ya 36
makadirio 2007
Uswidi0
makadirio 20060
makadirio 20071,006
Nafasi ya 87
makadirio 20070
makadirio 20071,006
Nafasi ya 50
makadirio 2007
Saint Lucia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Singapur0
makadirio 20060
makadirio 20076,600
Nafasi ya 51
makadirio 20080
makadirio 20076,600
Nafasi ya 25
makadirio 2008
Sierra Leone0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Slovenia0
makadirio 20064
Nafasi ya 90
makadirio 20061,105
Nafasi ya 86
makadirio 20060
makadirio 20071,073
Nafasi ya 48
2005
Saint Helena0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Shelisheli0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Saint Kitts na Nevis0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Saint Pierre na Miquelon0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Puerto Rico0
makadirio 20060
makadirio 2007736.2
makadirio 20070
makadirio 2007736.2
makadirio 2007
Guinea-Bissau0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Ureno0
makadirio 20060
makadirio 20074,112
Nafasi ya 60
makadirio 20070
makadirio 20074,095
Nafasi ya 33
makadirio 2007
Panama0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Paraguay0
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Nicaragua0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Antili za Kiholanzi0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Surinam0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Nauru0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Nepal0
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 2008
Vanuatu0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Niger0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Niue0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
New Caledonia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Maldivi0
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 2008
Malta0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Lebanon0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Laos0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Kiribati0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Korea Kaskazini0
20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Kenya0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Jamaika0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Iceland0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Honduras0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Luxemburg0
makadirio 20060
makadirio 20071,329
Nafasi ya 82
makadirio 20070
makadirio 20071,329
Nafasi ya 47
makadirio 2007
Lesotho0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Liberia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Hong Kong0
makadirio 20060
20083,080
makadirio 20080
20083,080
makadirio 2008
Haiti0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Guyana0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Guinea0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Guam0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Greenland0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Grenada0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Gibraltar0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Gambia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Polynesia ya Kifaransa0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Visiwa vya Faroe0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Visiwa vya Falkland0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Fiji0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Finland0
20060
makadirio 20072,268
Nafasi ya 75
makadirio 20070
makadirio 20074,576
Nafasi ya 30
makadirio 2007
El Salvador0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Eritrea0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Estonia0
makadirio 20060
20071,003
Nafasi ya 88
20070
20071,003
Nafasi ya 51
makadirio 2007
Jamhuri ya Dominika0
makadirio 20060
makadirio 2007250
Nafasi ya 94
makadirio 20060
makadirio 2007239.8
Nafasi ya 54
2005
Dominica0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Jibuti0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Cyprus0
20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Visiwa vya Cook0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Cape Verde0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Jamhuri ya Afrika ya Kati0
20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Costa Rica0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Komori0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Visiwa vya Cayman0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Sri Lanka0
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 20080
makadirio 2008NA
NA
Chad0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Kambodia0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Burundi0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Bhutan0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Belize0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Bosnia na Herzegovina0
20060
makadirio 2007400
Nafasi ya 92
makadirio 20060
makadirio 20070
2005
Bahamas0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Bermuda0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Armenia0
20060
makadirio 20072,050
Nafasi ya 78
makadirio 20070
makadirio 20072,050
Nafasi ya 42
makadirio 2007
Samoa ya Marekani0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
Antigua na Barbuda0
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 20070
makadirio 2007
KosovoNA
NA0
20070
2007NA
NANA
NA
LatviaNA
NA0
makadirio 20072,040
Nafasi ya 79
makadirio 20070
makadirio 20072,040
Nafasi ya 43
makadirio 2007
SenegalNA
NA50
Nafasi ya 81
makadirio 200650
Nafasi ya 102
makadirio 20060
makadirio 20070
makadirio 2007

Matumizi

Gesi huchomwa kama chanzo cha nishati kwa matumzi ya kibinadamu. Inachoma kwa kuonyesha ulimi wa buluu ambao ni safi hauachishi gesi nyingi za machafuko hewani.

Matumizi yake ni hasa

  • Uzalishaji umeme: gesi inapasha maji moto kwa kuendesha rafadha ya kuzalisha umeme
  • Upishi: gesi asilia hupatika ama kwa bomba hadi kila nyumba au katika chupa za gesi
  • Ukanzaji wa nyumba katika mazingira baridi
  • Fueli ya magari
  • Aina za plastiki hutengewezwa kwa gesi asilia

Gesi asilia husafiwa kwa sababu inachangia kidogo tu kwenye machafuko ya mazingira hasa kupanda kwa halijoto duniani. Hata hivyo si fueli bila machafuko. Pia sawa na fueli kisukuu nyingine akiba zake zinazidi kupungua haraka.

Kurasa nyingine

Marejeo

Viungo vya nje