Ganimedi (mwezi)

Ganimedi (ing. Ganymede) ni mwezi mkubwa zaidi wa Mshtarii (Jupiter) ambayo ni sayari ya tano kutoka kwa Jua na sayari kubwa katika mfumo wa Jua. Ni pia mwezi mkubwa katika mfumo wa Jua.

Ganimedi

Ukubwa

Kipenyo cha Ganimedi ni kilomita 5262 km hivyo ni kubwa kuliko sayari ya kwanza Utaridi (Mercury). Lakini ina nusu ya masi yake tu maana haina kiasi hiki cha densiti.

Kati ya miezi ya Mshtarii, Ganimedi iko kwenye nafasi ya saba ukihesabu kutoka sayari yenyewe.

Ganimedi inazunguka Mshtarii katika kipindi cha siku saba hivi. Obiti yake inashikamana na obiti za miezi Europa na Io katika uhusiano wa 1: 2: 4.

Ugunduzi na Jina

Ganimedi ni mmoja wa miezi ya Mshtarii iliyotambuliwa mnamo 7 Januari 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa mtu wa kwanza kutazama nyota kwa kutumia darubini. Hivyo inajulikana pia kama mwoja wa "miezi ya Galileo" maana iligunduliwa na Galilei pamoja na miezi 3 mingine ya Mshtarii na hayo yalikuwa magimba ya kwamnza yaliyoonekana kuzunguka sayari nyingine.[1]

Iliwahi kuitwa kwa majina mbalimbali. Jina lililobaki lilipendekezwa na mwanaastronomia Simon Marius. Kufuatana na desturi ya Ulaya kuziita sayari kwa majina ya miungu kutoka dini za kale, Marius alipendekeza jina la "Ganimedi" (gir. Γανυμήδης ganimedes) , kijana mpenzi wa mungu mkuu Zeu (sawa na Jupiter wa Waroma wa Kale) katika masimulizi ya Wagiriki. wa Jupita).

Muundo na tabia zinazojulikana

Muundo wa kudhaniwa wa Ganimedi kufuatana na data zilizopatikana hadi 2020

Kwenye kitovu chake kuna kiini cha metali kinachofikiriwa kuwa katika hali ya joto na kiowevu ambacho ni hasa chuma na nikeli. Myuko :en:convection ndani ya kiini hiki ni sababu ya kumkinika ya ugasumaku wake. Ganimedi hadi sasa ni mwezi wa pekee uliogunduliwa kuwa na ugasumaku.

Ganymede inadhaniwa imeundwa na miamba ya kisilika na maji. Uso wake wa miamba hufunikwa na bahari yenye kina cha kilomita mia kadhaa. Tabaka la juu la bahari hiyo limeganda, ni barafu. Kwa hiyo uso wote wa Ganimedi ni barafu[2]. Kuna makadirio ya kwamba kiasi cha maji kwenye Ganimedi kinazidi jumla ya maji Duniani.[3]

Uso unaonyesha maeneo meusi na maeneo meupemeupe. Sehemu nyeusi zinaonyesha kasoko nyingi kutokana na migongano na asteroidi ndogo, sehemu nyeupe zinaonyesha zaidi mabonde na safu za milima. Inadhaniwa kwamba sehemu nyesui ni za kale zaidi, na sehemu nyeupe zimepokea umbo kutokana na miendo ya gandunia .

Ugasumaku wa Ganimedi inadhaniwa umetokana na myuko (en:convection) ndani ya kiini chake cha chuma moto katika hali ya kiowevu[4].

Ganimedi ina angahewa hafifu sana ya inayonyesha oksijeni ambayo ni pamoja na O, O 2, na labda O 3 ( ozoni ). Viwangi vidogo vya hidrojeni vilipimwa pia kwwa njia ya uchambuzi wa spektra.

Uchunguzi

Picha iliyotumwa na Mariner 10 kwenye mwaka 1973

Mbali na kuiangalia kwa darubini, vipimaanga kadhaa waliongeza data na elimu kuhusu Ganimedi. Hadi sasa vyote vilitumwa na NASA ya Marekani:

  • Pioneer 10 ilipita kwa Ganimedi mwaka 1973 ikatuma picha ya kwanza ya mwezi huo ikafuatwa na Pioneer 11 mwaka 1974[5].
  • Voyager 1 na Voyager 2 vilifuata mwaka 1979. Viliweza kupima ukubwa wa Ganimedi vikatambua kuwepo kwa mabonde na milima

[6].

  • Galileo ilifika mwaka 1995 ilizunguka Mshtarii na miezi yake kwa miaka nane. Galileo ilipita mara kadhaa karibu na Ganimedi, safari moja kilomita 260 pekee juu ya uso wake. Iligundua ugasumaku na bahari ya maji iliyopo chini ya uso wa barafu[7]

+ New Horizons ilipita mwaka 2007[8]

Kipimaanga kinachopangwa kufuata ni JUICE (Jupiter Icy Moon Explorer) inayoandaliwa na mamlaka ya usafiri wa anga ya Ulaya ESA. Ilitarajiwa kurushwa mwaka 2022. Itahitaji zaidi ya miaka 7 kufika kwenye mfumo wa Mshtarii, itatangulia kupita kwenye miezi ya Europa na Kallisto hadi kuingia katika obiti ya kuzunguka Ganimedi mnamo mwaka 2032[9].

Ulinganishi wa ukubwa wa Dunia (kulia), Mwezi (juu), na Ganimedi (chini).

Marejeo

 

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: