Gerimani


Gerimani ni elementi yenye namba atomia 32 kwenye jedwali la elementi, uzani atomia ni 72,630. Alama yake ni Ge.

Gerimani
Jina la ElementiGerimani
AlamaGe
Namba atomia32
Mfululizo safuSimetali
Uzani atomia 72.64
Valensi2 na 4
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka1211.40  K (938.25 °C)
Kiwango cha kuchemka3106 K (2833 °C)
Asilimia za ganda la dunia6 · 10-4 %
Hali maada mango

Tabia

Gerimani ni dutu mango na katika mazingira ya kawaida ni metali ngumu yenye rangi ya kifedha-nyeupe. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 938.3 .

Ilitambuliwa mwaka 1886 na Mjerumani Clemens Winkler aliyebuni jina kwa heshima ya nchi yake ya kuzaliwa (lat. Germania)

Upatikanaji

Hupatikana mahali pengi ndani ya madini ya shaba na zinki kwa asilimia ndogo haitokei kiasili kama elementi tupu. Huchimbwa hasa China, Urusi, Kanada, Ufini na Marekani. Uzalishaji kwenye mwaka 2011 ilikuwa mnamo tani 100. Takriban theluthi moja ya uzalishaji wake ni kwa njia ya kurejeleza.[1].

Matumizi

Ilikuwa muhimu kama nusukipitishi katika vifaa vya elektroniki kama transista hadi silikoni imetumiwa zaidi badala ya Gerimani. Inatumiwa pia kwa kutengeneza vioo kwa ajili ya vifaa vya kuona nuru ya inforedi kama vile hadubini za usiku au kamera za inforedi.