S
Alfabeti ya Kilatini | |||||
---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | |
Ww | Xx | Yy | Zz | ||
(Kwa matumizi ya Kiswahili) | |||||
ch | dh | gh | kh | ||
mb | mv | nd | ng | ng' | nj |
ny | nz | sh | th |
S ni herufi ya 19 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Sigma ya alfabeti ya Kigiriki.
Maana za S
- katika kemia S ni alama ya sulfuri.
- Kwa magari S ni alama ya gari kutoka Uswidi.
- katika ya vipimo sanifu vya kimataifa "s" ni alama ya sekunde
Historia ya S
Kisemiti asilia alama ya meno | Kifinisia shin | Kigiriki Sigma | Kietruski S | Kilatini S |
---|---|---|---|---|
Asili ya herufi S ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na alama ya "shin" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya meno wakitumia alama tu kwa sauti ya "sh" na kuiita kwa neno lao kwa meno "shin". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "sigma" bila kujali maana asilia ya "meno". Kwao imekuwa sauti tu ya "s" kwa sababu hawakujua "sh".
Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi wakigeuza mwelekeo wake. Waroma wakaichukua kutoka hapa lakini walilainisha kona kali kuwa S jinsi ilivyo hadi sasa.