F

Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
AaBbCcchDd
EeFfGgHhIiJj
KkLlMmNnOoPp
QqRrSsTtUuVv
WwXxYyZz

F ni herufi ya 6 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni alama ya Digamma katika alfabeti ya Kigiriki ya kale.

Maana za F

Historia ya alama F

W ya Kisemiti asiliaW ya KifinisiaDigamma (W) ya KigirikiW ya KietruskiF ya Kilatini

Asili ya herufi F ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia. Alama ya F ina historia ambamo maana na matamshi yalibadilika mara kadhaa.

Wafinisia walikuwa na alama ya "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo wakitumia alama tu kwa sauti ya "w" na kuiita kwa neno lao kwa fimbo "waw". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma kwa sauti ya f au v na umbo la pili kama ipsilon bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Katika mabadiliko ya lugha ya Kigiriki matamshi ya "f/v" kabla ya vokali yalipotea hivyo hata alama ya digamma ilifutwa kama herufi ikabaki kama alama ya namba "6" tu.

Waetruski walipopokea alfabeti kutoka Wagiriki walikuwa na haja kwa sauti iliyopotea katika Kigiriki kwa hiyo walitumia digamma tena kama herufi. Walihitaji pia alama ya sauti "f" isiyopatikana katika Kigriki cha wakati ule. Waetruski walitumia digamma pamoja na alama ya pili kwa sauti ya F.

Waroma walipoendeleza alfabeti ya Kietruski walitumia tu sehemu ya kwanza ya "f" ya Kietruski yaani alama ya digamma. Kwa sauti ya "u" ma "w" waliwahi kuazima ile u-psilon ya Wagiriki. Kwa hiyo digamma imekuwa F ya Kilatini.