Wakurdi

Wakurdi (kwa Kikurdi: گەلی کورد, Gelî kurd) ni watu wanaotumia lugha ya Kikurdi, moja kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi[22] wanaoishi hasa Mashariki ya Kati.

Wakurdi
Kurd کورد
Roj emblem.svg
Watu kwa jumla
milioni 30–40 [1]


(The World Factbook, 2015 estimate)
milioni 36.4–45.6 [2]
(Kurdish Institute of Paris, 2017 estimate)

Maeneo penye idadi kubwa kiasi
Maeneo ambako Wakurdi wako wakazi asilia
 Uturukiest. 14.3–20 million[1][2]
 Uajemiest. 8.2–12 million[1][2]
 Iraqest. 5.6–8.5 million[1][2]
 Syriaest. 2–3.6 million[1][2]
Wakurdi nje ya maeneo ya asili (nje ya Kurdistan penyewe)2 million
 Ujerumani800,000[3]
 Ufaransa150,000[4]
 Uswidi83,600[5]
 Uholanzi70,000[6]
 Ubelgiji50,000[7]
 Urusi63,800[8]
 Ufalme wa Muungano50,000[9]
 Kazakhstan42,300[10]
 Uswisi35,000[11]
 Denmark30,000[12]
 Jordan30,000[13]
 Austria23,000[14]
 Ugiriki22,000[15]
 Marekani15,400
 Georgia13,861[16]
 Kyrgyzstan13,200[17]
 Kanada11,685
 Ufini10,700[18]
 Australia7,000[19]
 Azerbaijan6,100[20]
 Armenia2,162[21]
Makundi yaliyo karibu kiukoo au kiutamaduni

Other Iranian peoples

Kurdistan

Eneo lao linaitwa mara nyingi Kurdistan na limegawanyika kisiasa kati ya nchi za Uturuki mashariki, Iran kaskazini magharibi, Iraq kaskazini na Syria kaskazini.[23]

Hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Wakurdi wengi waliishi ndani ya maeneo ya Milki ya Osmani, idadi ndogo zaidi walitawaliwa na Uajemi. Milki zote mbili zilikuwa milki za Kiislamu ambako hakukuwa na mkazo wa utaifa au utamaduni maalumu. Hawakuwa na historia ya kujitazama kama taifa la pamoja wakiishi katika utaratibu wa jamii za kikabila zilizojitegemea na kutunza kiwango cha uhuru kutoka serikali za milki walimoishi.

Katika kongamano la kupatana amani baada ya Vita Kuu ya Kwanza suala la Wakurdi lilijadiliwa lakini bila kupata suluhisho. Waligawanywa tu.

Baada ya ugawaji wa Milki ya Osmani mwaka 1918 walijikuta katika nchi ambako watu wengi walikuwa ama Waturuki, Waarabu au Waajemi walioathiriwa na itikadi ya utaifa. Wakurdi waliambiwa kujitazama kama raia wa nchi hizo na hivyo kuwa Waturuki, Waarabu au Waajemi. Hasa ndani ya Uturuki chini ya rais wa kwanza Ataturk kuwepo kwa Wakurdi kulikanwa, wenyewe waliitwa "Waturuki wa milimani". pote walikataliwa kuwa na shule ambako watoto wao wangejifunza lugha ya Kikurdi.

Katika historia hii uko msingi wa upinzani wa Wakurdi uliotokea katika nchi zote wanapoishi kiasili.

Idadi

Idadi yao inakadiriwa kuwa milioni 30-45.[24] Ndilo taifa kubwa kuliko lote duniani lisilo na nchi huru ya kwao.

Lugha na dini

Lugha yao ni Kikurdi, chenye lahaja mbalimbali[25][26].

Wengi wao hufuata dini ya Uislamu (hasa madhehebu ya Wasunni), lakini wako pia wafuasi wa dini ya jadi wanaoitwa Wayazidi, wafuasi wa imani ya pekee ya Ahl-e Hak, halafu Wakristo, Wayahudi na Wazoroasta wachache.

Tanbihi

Vyanzo

  •  
  •  
  •  
  •  
  • Barth, F. 1953. Principles of Social Organization in Southern Kurdistan. Bulletin of the University Ethnographic Museum 7. Oslo.
  • Hansen, H.H. 1961. The Kurdish Woman's Life. Copenhagen. Ethnographic Museum Record 7:1–213.
  • Leach, E.R. 1938. Social and Economic Organization of the Rowanduz Kurds. London School of Economics Monographs on Social Anthropology 3:1–74.
  • Longrigg, S.H. 1953. Iraq, 1900–1950. London.
  • Masters, W.M. 1953. Rowanduz. Ph.D. dissertation, University of Michigan.
  • McKiernan, Kevin. 2006. The Kurds, a People in Search of Their Homeland. New York: St. Martin's Press. ISBN|978-0-312-32546-6
  •  
  • Matthee, Rudi. "ŠAYḴ-ʿALI KHAN ZANGANA". Encyclopaedia Iranica. http://www.iranicaonline.org/articles/shaykh-ali-khan.

Marejeo mengine

  • Samir Amin (October 2016). The Kurdish Question Then and Now, in Monthly Review, Volume 68, Issue 05
  • A People Without a State: The Kurds from the Rise of Islam to the Dawn of Nationalism, by Michael Eppel, 2016, University of Texas Press

Historia

  • Maxwell, Alexander; Smith, Tim (2015). "Positing 'not-yet-nationalism': limits to the impact of nationalism theory on Kurdish historiography". Nationalities Papers 43 (5): 771–787. doi:10.1080/00905992.2015.1049135. 

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Suala la Wakurdi nchini Uturuki