Namba za Kiroma

Namba za Kiroma (kwa Kiingereza: Roman numerals) ni mfumo wa tarakimu kwa kuandika namba jinsi ulivyokuwa kawaida wakati wa Roma ya Kale na katika mwandiko wa Kilatini. Mfumo huu unaendelea kutumika hadi leo kwa namba za pekee, hasa katika muundo wa orodha ambako mgawanyo ni wa ngazi mbalimbali. Ni kawaida kwa kutofautisha watu wenye jina lilelile, kwa mfano wafalme au mapapa: Malkia Elizabeth II (= wa pili) au Papa Benedikto XVI (= wa kumi na sita).

Herufi za alfabeti kama tarakimu

Jinsi ilivyo katika lugha mbalimbali, hata Waroma walitumia herufi za alfabeti ya Kilatini (ingawa chache) kama tarakimu za kutaja namba pia.

Alama za kimsingi

Herufi chache zilizotumika kwa namba muhimu zaidi, ambazo ziunganishwe kupata namba zote, ni:

I - 1

V - 5

X - 10

L - 50

C - 100

D - 500

M - 1000

AlamaNambaAlamaNambaAlamaNambaAlamaNambaAlamaNambaAlamaNambaAlamaNamba
I1V5X10L50C100D500M1000


Kuunganisha alama za namba

Kujumlisha alama

Namba kubwa zaidi huonyeshwa kwa kuandika alama inayotakiwa upande wa kulia lakini kwa kawaida si zaidi ya mara tatu:
I = 1; II = 2; III = 3, V ni 5 lakini VI ni 6; XX ni 20 lakini XXI ni 21.

Walikuwa na utaratibu wa kutoandika zaidi ya alama tatu ya aina ileile mfululizo. Lakini waliweza kupuuza utaratibu huu pia na kuandika VIIII (9) badala ya IX au XXXX (40) bafala ya XL.

Kupunguza alama

Namba ndogo zaidi huonyeshwa kwa kuandika alama ndogo upande wa kushoto:
V ni 5 lakini IV ni 4 badala ya IIII (inayotokea mara chache); X ni 10 lakini IX ni tisa

Hapa walifuata utaratibu ufuatao:kuweka I moja au X moja au C moja tu kabla ya alama kuwba zaidi; halafu namba hii yatolewa kwenye namba kubwa:

Mfano: IX=9; IXX = 19; IL = 49; LIV=54; XC=90; CD=400; CM=900

I pekee huwekwa kabla ya V au X; X pekee kabla ya L au C; C pekee kabla ya D au M.

Mfano: XCIX (99) lakini siyo IC; CMXCIX (999) lakini siyo IM

Namba mfululizo 1-100

IIIIIIIVVVIVIIVIIIIXX
12345678910
XIXIIXIIIXIVXVXVIXVIIXVIIIXIXXX
11121314151617181920
XXIXXIIXXIIIXXIVXXVXXVIXXVIIXXVIIIXXIXXXX
21222324252627282930
XXXIXXXIIXXXIIIXXXIVXXXVXXXVIXXXVIIXXXVIIIXXXIXXL
31323334353637383940
XLIXLIIXLIIIXLIVXLVXLVIXLVIIXLVIIIXLIXL
41424344454647484950
LILIILIIILIVLVLVILVIILVIIILIXLX
51525354555657585960
LXILXIILXIIILXIVLXVLXVILXVIILXVIIILXIXLXX
61626364656667686970
LXXILXXIILXXIIILXXIVLXXVLXXVILXXVIILXXVIIILXXIXLXXX
71727374757677787980
LXXXILXXXIILXXXIIILXXXIVLXXXVLXXXVILXXXVIILXXXVIIILXXXIXXC
81828384858687888990
XCIXCIIXCIIIXCIVXCVXCVIXCVIIXCVIIIXCIXC
919293949596979899100